Shetta ajibu chanzo cha bifu lake na Diamond Platnumz - SHINE MUSIC TZ

Sunday, 10 December 2017

demo-image

Shetta ajibu chanzo cha bifu lake na Diamond Platnumz

Shetta+na+Diamond

Msanii wa muziki Bongo, Shetta amefunguka kuhusu madai ya kuwa na beef na Diamond.
Shetta ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Vumba’ ameiambia The Playlist, Times Fm kuwa hawana beef ila kilichotokea ni kila mmoja kujikita zaidi katika kazi zake na kuacha kufanya kazi kishkaji.
“Sidhani kama nina tatizo na Diamond na yeye hana tatizo na mimi, nafikiri ubize na kila mtu ana shughuli nyingi” amesema Shetta.
“Kuhusiana na kazi nafikiri ni mambo ya management, unajua mwanzo tulikuwa tunafanya kazi kishakaji sana, sasa imekuja biashara, yeye anapata hela na mimi napata, so nafikiri sasa hivi management hazina ule ushikaji sana, tumekaa kibiashara kitu ambacho ni kizuri” amesisitiza.
Shetta ameongeza kuwa hata wimbo wake ‘Wale Wale’ upo katika mtandao wa wasafi ambao ni wa Diamond kitu ambacho kina hashiria hawana ugomvi wowote.

Utakumbuka wawili hawa walishafanya ngoma mbili pamoja ‘Nidanganye na Shikorobo’ zote zikiwa za Shetta


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *